KISIMA CHA MATATIZO:
SURA YA KWANZA:
‘’Nikweli najua ipo siku nitasahau shida zangu zote,
lakini kwasasa naona giza sijui namna ya kutatua matatizo niliyonayo!’’ mbaya
zaidi kila likiisha moja linaanza jingine, sijui ni mkosi au laana’’ ilikua ni
sauti ndogo yenye mvuto lakini ilitoka kwa kukata kata toka kwenye midomo
mipana yenye mvuto, kwasasa urembo wake ulikua umejificha kutokana na simanzi
na machozi yaliyokua yakitiririka mashavuni mwa binti huyu, Alikua akiitwa
Pamela, lakini wengi walifupisha jina lake na kumuita Pam, Alikua ameketi
kwenye kochi moja lililokua chumbani humo, kwenye kochi la jirani yake ailikua
amekaa Mary, mary alikua rafiki yake na Pamela toka wakiwa shule ya msingi.
Chumba hiki walichokua wamekaa Pamela na Mary, ilikua ni nyumbani kwa akina
Mary aliyekuwa akiishi na dada yake na shemeji yake.
*****
Lucy alikua ni motto wa pekee toka kwenye familia ya Mzee
Peter Mihambo, wa mjini Mwanza maeneo ya Magu, Mzee Peter alikua ni Mzee mwenye
uwezo kijijini na pia alikua na elimu ya kutosha kwa wakati huu alikua
amestaafu lakini alikua akimiliki mifugo
pia alikua akimiliki boti ndogo kwa ajili ya shughuli za uvuvi Ziwa Victoria,
hayo yote yalimpa heshima pale kijijini, wazee wenzie walikua wakimuita Mzee
PETERI.
Kwa wakati huo Lucy alikua darasa la sita katika shule ya
msingi magu. Lucy alikua na maendeleo mazuri sana shuleni toka akiwa darasa la
kwanza, pia alikua ni motto mwenye tabia nzuri jambo lililompa heshima pia Mzee
Peter, Mzee Peter mara kwa mara alimweleza binti yake ata hakikisha amemsomesha
mpaka ngazi ya juu ya elimu, hata kama itamlazimu kuuza mifugo yake yote.
Ingawa Lucy alikua darasa la sita tu
wakati huo lakiniuzuri na urembo wake haukujificha, Lucy alikua mzuri wa sura
na hata umbo lake lilifinyangika vizuri na rangi yake ya maji ya kunde
iliongeza chachu zaidi, kama yangefanyika mashindano ya ulimbwende basi Lucy
angenyakua taji bila mjadala.
Kama ilivyokua kwa Mzee Peter, mama mzazi wa Lucy Bi.
Imelda hakua nyuma katika kumpa malezi bora binti yao Lucy, na hata ilipobidi
kuwa mkali alikua mkali ili tu binti yao asije kuingia kwenye vishawishi vya
ulimwengu huu. Na kwa wakati huo tatizo la kijijini pale ilikua mabinti wengi
kushindwa kumaliza shule au kumaliza wakiwa wajawazito. Mzee Peter pia alikua
mkali kwa binti yake juu ya swala hilo, alikua akimweleza binti yake kua kama
atamuaibisha kwa swala hilo basi atahakikisha anamtenganisha kichwa na kiwili
wili.
SURA YA PILI:
Wataalam wa mambo wanasema karibu wanawake wote hawana
‘’wazo la pili’’ (second thought). Kwa bahati mbaya sana, Hata Lucy alijikuta
akiingia kwenye kundi hili la wasio kua na wazo la pili. Alikua darasa la saba
akajikuta ameshawishika na kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwalimu
wake wa darasa kwa ahadi kua atamuuibia mtihani wa mwisho wa kuhitimu darasa la
saba. Lucy kwa wakti huo alifikiri juu ya kuibiwa tu mtihani akasahau kuwaza
kuhusu madhara ya uhusiano huo wa kimapenzi.
Lucy aliendelea na uhusiano huo wa kimapenzi na mwalimu
wake wa daras, Mwalimu Dennis, bila mtu yeyote kugundua . ilikua ngumu sana
kugundulika kwani Lucy alikua karibu sana na walimu wake karibu wote tofauti na
wanafunzi wengine walio kua wakiwaogopa walimu. Siku zote za mwizi ni arobaini,
miezi miwili kabla hajaitimu elimu yake ya shule ya msingi, walikuja wageni shuleni
kwao kutokea wizara ya afya, ugeni huo uliendesha zoezi la kuwapima ujauzito
wanafunzi wote wa kike wa darasa la saba, ndipo ilipogundulika wanafunzi
ishirini wanaujauzito akiwemo Lucy, aliyekua na ujauzito wa mwenzi mmoja.
Taarifa zilifika nyumbani kwa akina Lucy, kwa bahati baba yake na Lucy hakuwepo
nyumbani, alikua amekwenda kisiwani ukerwe kwa shughuli za uvuvi, hivyo taariza
za ujauzito zilimfikia mama yake Lucy bi. Imelda. Mama yake Lucy alipatwa na
simanzi sana, lakini siku zote motto kwa mama hakui, nawahenga walisema Mtoto
akinyea kiganja huwezi kukikata. Bi Imelda alimuonea huruma binti yake,
akamuuliza mhusika wa ujauzito huo ni nani. Lucy bila kumficha mama yake
akamueleza ukweli wote, mama yake alimpa pole kasha akamuuliza lakini mwanangu
unakumbuka baba yako alikua akikueleza nini kuhusu swala hili endapo
litatokea,? Lucy hakuweza kujibu alivuta pumzi na kujiinamia kabla ya kuangua
kilio kikubwa kilichoaambatana na kwikwi, Lucy alikua akijuta lakini siku zote
majuto ni mjukuu, Lucy alilia kwa mambo mawili kama sio matatu, la kwanza
ilikua kukatiza masomo yake, lapili ilikua mhusika wa ujauzito huo, mwalimu
denis alikutwa amejinyonga chumbani kwake kuhofia mkono wa sheria na la tatu
ilikua ni hatua ambayo baba yake angechukua mara baada ya kurejea. Bi Imelda
alinyanyuka alipokua mekaa akamfuata mwanae, akamsogelea akaanz kumfuta
machozi, akamwambia nyamaza binti yangu, maji yakisha mwagika hayazoleki,
naomba unyamze na usikilize kwa makini sana, akaanza kuongea huku amemkazia
macho kidogo binti yake akamwabia ‘’ namfahaamu mzee mihambo akisema jambo
lake, amesema’’ hivyo mwanangu kuna wazo limenijia kichwani itabidi nikutoroshe
mpaka pale baba yako hasira zitakapopungua, kuna akiba yangu iliyokua
nimehifadhi itabidi nikupatie kesho asubuhi nikutoroshe uende dar, ukamtafute
mama yako mdogo atakusaidia, kinyume na hivyo baba yako akikukuta hapa atakuua
kweli. Bi Imelda alimkumbatia mwanae akamwambia ajiandae kwasafari alfajiri
iliyofuata kwani usiku ulikua umeshaingia. Kwa kweli usiku huo haukua mzuri
sana kwa Lucy, alilala usingizi wa mangam ngam na mara nyingine kuota ndoto za
kutisha tisha, Hauchi hauchi, unakucha hatimae alfajiri ilifika, bi Imelda
alimtorosha bintie, bila watu kumuona na Lucy akapanda treni kuianza safari
yakuelekea dar, njiani alionekana mwenye mawazo sana na wakati mwingine
alijisahau na kuanza kulia kabisa,
******
Jioni ya siku hiyo hiyo aliyotoroshwa Lucy, ndio mzee
mihambo alirejea nyumbani akitokea ukerewe kwenye shughuli zake za uvuvi.
Tofauti na siku zote nyingine alizokua akipata mapokezi bashasha toka kwa mke
wake kipenzi kila lipotoka safari, hata kama ingekua safari fupi, siku hiyo
hakupata mapokezi yeyote toka kwa mkewe. Bi Imelda alikua amejiinamia mbele ya
nyumba yao, huku akionekana mtu mwenye masikitiko na majonzi, hukua akionekana
mtu aliyeshinda akilia, Bi Imelda alipomuona mume wake, alijizoa zoa kutoka
mahala alipokua amekaa na kumpoke mumewe, Mzee Mihambo kabla ya kuingi ndani ya
nyumba aligundua mambo hayakua shwari nyumbani kwake. Mzee Mihambo alimuuliza mkewe
‘’ kuna usalama kweli hapa mke wangu?’’ Bi Imelda hakuweza kuongea chochote,
zaidi ya kutokwa na machozi, ndipo alipojikaza na kumjibu mumewe. Kua aingie
ndani kwanza, aoge na kupumzika kwanza ndipo atamueleza yaliyojiri akiwa
safarini. Baada yam zee Mihambo kuoga na kupumzika ndipo alipokaa na mkewe, Bi
Imelda alimueleza mumewe yote yalijiri kwa kipindi hicho ambacho hakuwepo
nyumbani na alipofika kwenye mada ya ujauzito wa Lucy, alijikuta akilengwa
lengwa na machozi, akavuta pumzi kasha akazishusha akaendelea kumueleza mumewe
kua kilichomsikitisha zaidi kuwa Lucy ametoroka na hajui amekwenda wapi (
alimdanganya mumewe) mzee mihambo aliinamisha kichwa chini kwa muda, na
alipokinyanyua alikua amebadilika, uso wake ulionyesha hasira na dhahiri macho
yake yalikua mekundu, ndipo akamwangalia mkewe kwa macho makali na kumwambia
kua, yeye ndiye anayejua siri yote ya binti yake, akamwambia atagundua ukweli
wote na kusema kua afadhali amemtorosha binti yake mapema, maana kama angemkuta ingekua ndio mwisho wa maisha
yake. Baada ya kuyasema hayo, Mzee Mihambo alinyanyuka na kuondoka kwa hasira.
Bi Imelda alibaki aikwa amejiinamia huku akilia kwa kwikwi.
*******
Ilikua ni ndani ya treni, masaa yalikua yamesogea sana
toka treni hiyo ilipo acha viunga vya stesheni mjini Mwanza. Abiria walikua
wakiendelea na shughuli mablimbali wengine walionekana wakipiga hadithi za hapa
na pale wengine midomo ilionekana ikitafuna na wengine walikua wamesinzia,
Kwenye Treni hiyo ndipo alipokuwemo Binti Lucy, tokea safari ilipoanza mjini
mwanza, alionekana akiwa mwenye mawazo mengi sana, pembeni yake alikua ameketi
dada wa makamo kidogo, dada huyo alionekana kumfuatilia Lucy toka safari
ilipoanza, Dada huyo aliamua kuvunja ukimya, akamuuliza ‘’samahani mdogo wangu
mbona unaonekana mwenye mawazo sana, natoka safari ianze sijakuona ukila
chochote?’’ Lucy hakuweza kujibu chochote zaidi ya kutiririkwa na machozi, dada
Yule hakuchoka kumwambia ‘’Pole dada unaonekana unamatatizo, samahani kama
nakukwaza mimi naitwa dada Patricia, ingawa wengi wananiita Sia, ni mfanya
biashara, naishi dar, maeneo ya magomeni mwembechai’’ ndipo Patricia alipotoa
keki mbili na kumpatia Lucy akimwambia apooze njaa, Lucy alimshukuru dada Yule
kwa ukarimu wake. Lucy alijitambulisha kwa Patricia kua yeye alikua akiitwa
Lucy. Na ni motto yatima, na pale mwanza alikua akifanya kazi za ndani, ndipo
alipobakwa na kupewa ujauzito (Alimdanganya) hivyo anakwenda jijini dar
kumtafta mama yake mdogo aliyekua akiishi maeneo ya manzese, Lucy alitoa picha
aliyopewa na mama yake ikiwa na sura ya mama yake mdogo huyo, aliyemwambia
Patricia kua alikua akiitwa Daniella. Patricia aliangalia picha ile kasha
akamgeukia Lucy, akamwambia ‘’Pole sana mdogo wangu kwa yote, lakini kwa jiji
kubwa kama dar kumtafuta ndugu yako kama huyo itakua ngumu, ila usijali nina
rafiki yangu anayeishi maeneo ya manzese hivyo basi tutakapofika dar,
nitakupeleka kwa rafiki yangu huyo, umsaidie kwenye biashara yake ukiwa
unaendelea kumtafuta mama yako mdogo. “ Lucy alifurahishwa na hatua hiyo
akamshukuru Patricia’’
SURA YA TATU:
Ilikua ni taarifa ya habari ya saa nne asubuhi, ndipo
mtangazaji aliporipoti tukio la kusikitisha lililotokea mjini mwanza usiku wa
kuamkia siku hiyo. Mtangazajia aliripoti kua familia moja mjini mwanza, maeneo
ya Magu wamekutwa wameuwawa kufuatia kuchomwa moto nyumba yao na mifugo yao na
watu wasiojulikana, wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na uchunguzi zaidi
unaendelea, kujua ukweli wa tukio hilo la kinyama. Mtangazaji aliporipoti kua
watu waliouwawa ni Mzee Peter Mihambo na mkewe bi Imelda mihambo. Wakati huo
Lucy na Patricia walikua tayari wako kwenye daladala lililokua likitokea
stesheni kuelekea ubungo, jijini dar, wakati taarifa ya habari hiyo ikiendelea
ndipo Lucy alipoangua kilio, Patricia akamuuliza Lucy ‘’Vipi unawafahamu au?’’
Lucy hakuweza kujibu chochote, kwasababu alishamdanganya kPatricia kua yeye
alikua motto yatima, ingawa taarifa hiyo ilimuuma sana mpaka bado kidogo aseme
ukweli, lakini kwa wakati huo hakua na kitu chakufanya, kondakta wa gari hiyo
aligonga akauliza kama kuna mtu aliyekua akishuka manzese, ndipo Patricia
alipomshtua Lucy kua wamefika hivyo wateremke, Lucy alikua ameishiwa nguvu
kabisa lakini alijikaza, wakateremka kutoka kwenye gari hiyo. Patricia
alimuongoza Lucy na kuingia mitaa kadhaa iliyokua ndani ndani ya manzese kabla
hawajakaribia nyumba moja chakavu kidogo iliyokua na vibanda viwili vya mabati
machakavu kidogo pia. Patricia akamwambia ‘’tunapokwenda ndio pale,
tumeshafika, futa basi hayo machozi’’ Lucy akawa ni kama mtu aliyetoka
usingizini, baada ya kuyasikia maneno hayo toka kwa Patricia! Maana alikuwepo
kimwili tu, mawazo yake yote hayakua pale, yalikua kwa wazazi wake mwanza na
kichwani mwake aliisikia ile sauti ya mtangazaji ikiripoti tukio la mauaji ya
wazazi wake ikijirudia rudia. Hawakupiga hata hatua tano wakawa wamesimama
mbele ya nyumba ile, Patricia akatangulia ‘’Hodi Hodi Shoga yangu’’ sauti
ikajibu ‘’Karibu shoga yangu Sia’’, Kutokea kwenye kibanda cha upande wa kulia
akatoka dada wa makamo kidogo kama Patricia akawakaribisha ‘’Karibuni ndani,
naona ndio mwaingia, namalizia kumpimia mteja supu naja.’’ Patricia akamuongoza
Lucy kuingia ndani ya nyumba hiyo ingawa ilikua asubuhi lakini ndani humo
kulikua na giza kutokana na madirisha ya nyumba hiyo kua madogo. Patricia
akamkaribisha Lucy kwenye kochi lilikoua ndani humo ‘’Karibu mwaya uketi, ndio
dar hii, hapa ndio utakapokua unaishi, ndio kwa Yule rafiki yangu anayeitwa
Rehema, anaroho nzuri tu, hivyo najua mtaishi vizuri tu, au sio mdogo wangu
Lucy?’’ Lucy akajibu ‘’ ndio dada yangu’’ zilipita kama dakika tatu za ukimya
ndipo Rehema akaingia ndani humo na kuvunja ukimya huo ‘’Habari za safari
jamani?’’ ‘’nzuri. Sijui za huku kwenu?’’ ‘’Ahaaa!! Njema, kama unavyotuona,
tunaganga ganga’’ ‘’sasa rafiki yangu rehema bila ya kupoteza mda, huyu anaitwa
lucy, nimekutana nae kwenye treni-mwanza, akanieleza matatizo yake, nikaona
nije nae hapa akusaidie shughuli zako, akiwa anamtafta mama yake mdogo, hiyo
nikwa ufupi tu, mengi zaidi atakueleza mwenyewe au wewe unaonaje?’’ ‘’kweli!!,
Lucy karibu mwaya, jisikie upo nyumbani, tutasaidiana kwa kila hali, matatizo
ni sehemu ya maisha mdogo wangu’’ Lucy aliwashukuru wote kwa pamoja, Patricia
nae hakukaa sana akawaaga na kuondoka. Basi ukawa mwanzo wa maisha mapya ya
Lucy jijini dar, akawa akimsaidia rehema kuuza supu na pombe katika vilabu
vyake, rehema alikua na moyo mzuri, alimchukulia Lucy kama mdogo wake kabisa,
taratibu taratibu kadri siku zilivyokua zikisogea, Lucy akajikuta akisahau
mambo ya Mwanza na kuzoea dar, na pia kuzoea hali yake ya ujauzito. Kiufupi
aliamua kumuachia Mungu mambo yake yote, hali hiyo ilimfanya Lucy anawiri na
uzuri wake uonekana dhahiri. Lucy akaanza kupata vishawishi vya hapa na pale
kutoka kwa wanaume waliokuwa wanakuja kama wateja na hata ambao hawakua wateja.
Lakini Lucy alikua na msimamo mpya hakua anataka mwanaume yeyote amshawishi
wala kumchezea mwili wake, na kwakiasi Fulani aliweza kuwadhibiti, kwani
wanaume wote waligonga ukuta.
*****
Nilihisi kama umeme fulaniukinitembelea mwilini, pale
aliponikumbatia kwa nyuma, maneno yake yalitetemesha ngoma za masikio nyangu
pale aliposema ‘’Hivi ni kweli Lucy hunipendi?’’ hebu niangalie usoni na
uniambie hunipendi’’ Nilijibaraguza
nkamgeukia badala ya kufuata alichonieleza, nikamwambia kwa aibu aibu huku
nikikwepesha macho ‘’Hivi Andrwe nani alikupa idhini ya kunikumbatia?’’ Kwa mara ya kwanza nilihisi nikimpenda
Andrwe. Mwanaume ni Mwanaume tu, alipuuza niliyomwambia akanishika mkono
tukaketi kwenye Bechi moja lililokuwepo kibandani mle, kulikua hakuna wateja.
Kwa sauti ya ukakamavu na kujiamini akaniambia ‘’Sijui kwa nini huniamini
Lucy,’’Mimi nipo tofauti sana na hawa wanaume wengine wa hapa, Lengo langu sio
kukuchezea au kukutumia kwa starehe za muda mfupi, lengo langu nahitaji tuanze
kuishi pamoja kama mume na mke, nielewe Lucy nakupenda’’ alipofikia hapo
aliongea kwa masikitiko zaidi huku akiniangalia machoni, kwa aibu za kike nikainamisha kichwa
chinihuku niking’ata kucha,nikaanza kumjibu kike kike,nikamwambia itakua ngumu
kwanza ni mdogo alafu ninaujauzito utakubali vipi kule ujauzito na mototo ambaye sio wako, alafu hapa
DSM sina ndugu yoyote, Dada Rehema ndio kila kitu kwangu kwa hio itakuwa
ngumu.Baada yakuyasema hayo nikajua atasimama na kuondoka lakini badala yake,
Akaniambia ‘’Sikiliza Lucy mimi nakupenda sana na waswahili walisema ukipenda Boga upende na Ua lake
hivyo wala usitilie shaka kuhusu ujauzito na mengine yote Patrisia
ameshanieleza ‘’ Nikashtuka kidogo nikamwambia na Patrisia unamfahamu? Akajibu
‘’Ndio’’ akaendelea akaniambia ‘’Kwa hio Lucy swala lipo kwako kama wewe
umekubali basi mwambie dada yako Rehema atakachosema utanieleza’’ sawa?’’ Kabla
sijajibu Dada Rehema akatokea Eeeh
Andrwe hujaenda tu,au umeniletea kreti jingine la bia, la ofa, iwe heri tu hapo na mdogo
wangu, maana nyie wanaume msione’’ Andrwe
hakusema kitu zaidi ya kutabasamu na kuondoka zake.
******
Siku hio Lucy alishinda akiwa na furaha kweli hata kazi
zake siku hio alizimaliza mapema kweli, ukweli ni kwamba hata yeye alihisi
kumpenda Andrwe. Usiku akiwa anajiandaa kulala, akaona ni vyema amueleze dada
yake Rehema, Basi Lucyakaamua kumueliza ukweli wote Rehema. Rehema akamwambia
Lucy ‘’Sikiliza Lucy wanaume hawaaminiki, lakini huwenda hii ikawandio bahati
yako.’’ Kwa jinsi mimi ninavyomfahamu Andrwe sio mtu mbaya labda abadilike, hivyo
basi kama wewe mwenyewe umeridhia basi mkubalie ombi lake, Kama utaenda huko na
yatakushinda basi jirudie hapa sasa ni kama nyumbani kwako, hivyo tuombe heri tu. Lucy alifurahishwa sana
na maneno hayo, wote wakatakiana heri ya usiku mwema na wakalala.
Baada ya majuma mawili kupita, Lucy alihamia rasmi
nyumbani kwa Andrwe, Lucy alishangaa sana alipofika nyumbani kwa Andrwe, Andrwe
alikua amejitahidi sana kimaisha, Ingawa alikua amepangisha chumba kimoja tu,
lakini kilikua kikubwa na kilikua kinavitu vyote ambavyo mwanaume anayeanza
maisha anatakiwa awe navyo. Kulikua na kitanda kikubwa cha 5 kwa 6, kabati la
nguo, makochi, kabati la vyombo, meza, stuli, Redio kubwa, na friji ngodo huku
sakafuni kukiwa na zulia matata [kipindi kile TV zilikua hazijaenea sana lakini
huenda angekua nayo] Hivyo vyotevilimchanganya sana Lucy, Lucy akamuuliza
Andrwe’’ Vijana wote hapa Magomeni ni matajiri kama wewe au?’’ Andrwe
akamuuliza kwa nini? Si vitu vyote vya thamani sikutegemea! Andrwe akamjibu
akamwambia ni uaminifu tu ndo ulinifanya niwe hivi, Huyu Bosi wangu nilianza
kazi kwenye baa yake kama weita tu lakini kwa sababu ya uaminifu ndio maana
ameniachia nisimamie kabisa baa yake pamoja na kusambaza vinywaji sehemu
mbalimbali kama ilivyokua pale kwenu. Lucy alimpongeza sana Andrwe na Andrwe
akamkaribisha Lucy hapo rasmi kama mke wake. Ikawa mwanzo mwingine mpya na
mzuri kwa Lucy.
SURA YA NNE
Ikawa imepita miaka 15 toka Andrwe na Lucy waanze kuishi
pamoja, kwa sasa hawakua wawili tena bali walikua familia, Lucy alikua sio Lucy
tena alikua akiitwa mama Pamela, Ilikua familia yenye furaha na maendeleo,
walikua bado wakiishi Magomeni. Andrwe alikua kichwa imara cha familia hiyo
kwani ndani ya miaka 15 hiyo familia ilikua imejaa furaha na Amani, pia Andrwe
alipanga kumpatia mkewe kazi kwenye baa ile aliyokuwa akifanyia kazi,pia
alikuwa akimsomesha Pamela na kwa sasa Pamela alikua kidato cha kwanza katika shule
ya sekondari Jangwani. Pamela alikua binti mzuri na mwenye tabia njema na bidii
katika masomo, mara nyingi alikuwepo nyumbani na kama usipomkuta ametumwa au
anajisomea kwa rafiki yake Mary alikua akiishi mtaa wa pili toka kwa akina
Pamela, Mary alikua rafiki kipenzi wa Pamela,walikuwa wakisoma wote shuleni
Jangwani. Mary alikua akiishi na dada yake n shemeji yake.
Licha ya familia ya kina Pamela kuwa na faraha lakini
kulikua na matatizo macchache ambayo wakati fulani yangeweza kufanya furaha
hiyo iyeyuke na kuleta majonzi kwa wahusika. Lucy toka alipomzaa Pamela
hakuweza kubeba ujauzito tena na baadhi ya madaktari kuwaLucy asingeweza kubeba
ujauzito tena. Hilolilikua tatizo kati ya Andrwe na Lucy, lakini ukiacha hilo,
Luch ni mara nyingi sana alisongwa na msongo wa mawazo,swala lililokua
linamtatiza kwambaamwambie au asimwambie au aendelee kumficha mpaka lini Pamela
kuwa Andrwe sio baba yake mzazi. Maswala haya kwa namna moja au nyingine
yalikuwa yakiitatiza familia hii.
*****
Ilianza kama utani, ilikua ni jioni moja Lucy akiwa
ametoka kazini, alianwa na maumivu ya tumbo yaliyokua makali sana,kiasi kwamba
machozi yalikua yakimtoka,Pamele alikua kasharudi pia kutoka shuleni na alikua
akiishuhudia hali ya mama yake, Alivyoona inazidi kua mbayaaliona ni bora
amfuate baba yake kazini ili wampelrke mama hospitali, Andrwe aliofika nyumbani
alishangaa sana kumkuta mke wake akiwa kwenyw hali ya maumivu makali wakati mda
mfupi tu umepita alikua kazini mzima kabisa. Ikambidi tax nakumkimbiza zahanati
iliokua karibu na mtaani kwao, walipofika Lucy aliingizwa moja kwa moja
daktari. Kutokana na hali aliyokua nayo ilibidi aandikiwe kulazwa. Ilibidi
Pamela na baba yake warudi nyumbani.