Wednesday, February 13, 2013

ZAWADI YA SANDA-1



ZAWADI YA SANDA.

Bado ni giza x 2, sioni wapi pakupapasa naishangaa sayari hi…’’ ulikua ni wimbo uliokua ukisikika toka chumbani kwa kijana Johnson kwa wafuatiliaji wa muziki watakua wameshajua wimbo huu ni wa nani, si mwingine ni kijana Matonyaaliyekua akivuma kipindi hicho, Hakika ilikua Tonya time. Licha ya wimbo huu kusikika kwa sauti ya juu, lakini wala kijana Johnson hakuwa akiusikia, kiganja chake kilikua bize kikichezea simu yake ndogon ya kiganjani na alikua amezama kwenye lindi zito la mawazo si kwakua alikua bize na simu la hasha! Kwani hata alichokua akikifanya kwenye simu hakukielewa, kiukweli akili yake ilikua haijatulia kabisa, Alikua ameketi kwenye sofa iliyokua chumbani humo, mbele yake sakafuni kulikuwa na mwili wa mwanamke ukiwa umelala haujitambui. Harufu ya kifo ilikua ikinukia!!! Akili ya Johson ilifanya kazi haraka sana, akaamua kumpigia simu rafiki yake David waliyekua wakiishi nae kwenye kota hizi za kupangisha maeneo ya Ntana, katika mji wa Kithithua. Siku ya kufa nyani miti yote huteleza alijisemea Johnson, pale alipokua amempigia simu David mara kadhaa lakini simu haikupokelewa, Johson alizidi kuchanganyikiwa kwani pia haikua kawaida ya David kuchelewa kurudi hadi usiku huo, Aliamua kujaribu kwa mara nyingine kuipiga simu hiyo ya swaiba yake! Kama mara kadhaa zilizopita simu hiyo iliita tu pila kupokelewa, mara nyingine tena akajaribu ikaitaa kwa muda mrefu lakini kabla haijakatika ikapokelewa upande wa pili…!

*****
Ulikua ni mgahawa mkubwa uliokusanya watu mbali mbali wa mjini pale, kutokana na kua katikati ya mji wa Kithinthua na pia bei za mgahawa ule zilikua ni za wastani hivyo kila mtu wa kuanzia kipato cha wastani aliweza kumudu kuingia mgahawani pale palipokua pia panaongoza kwa huduma na chakula kizuri kilichosifiwa na wengi, ndipo hapa Johson alipokutana na mwanadada Mary Limuli aliyekua mhudumu wa mgahawa huu wa Chichechi City Garden, ilianza kama utani kwa wawili hawa kuzoeana na hatimae kutumbukia kwenye dimbwi la mahaba mazito.

Johson alikua ni mwalimu katika chuo kimoja maarufu mjini Kithinthua, kilichojulikana kama Ville Technology College. Johnson alikua kijana mtanashati, mchapa kazi na mtu wa kujituma sana, ingawa walio wengi walikua wakisema Johnson alikua akiringa lakini ukweli alikua akionekana tu hivyo lakini sio uhalisia wake kwani alikua hana majivuno, mtu wa utani na mizaha ingawa hili usingeweza kulitambua mpaka umemzoea na kukaa nae kwa mda kidogo, wahenga walisema kizuri hakikosi kasoro ndivyo alivyokua pia Johson kwani kasoro yake kubwa ilikua ni kupenda wanawake, vijana wanasema alikua mzee wa totoz!! Ni tabia hii iliyokuja kumuingiza matatizoniingawa mwenyewe alikua akijigamba kua alikua mzee wa mapenzi ya kigumu, au Gengstar Loving kwa lugha ya wamarekani weusi, Wanawake wake wengi alikua akienda nao kula kwenye mgahawa wa Cichechi City Garden, kitu alichokua akikifanya bila kujua kua alikua akimuumiza Mary, Mary alikua amempenda Johson toka siku ya kwanza alipomuona, lakini ilikua ngumu kumueleza ukweli, aliishia kumtania tu,
Ilikua ngumu kwa Mary kumueleza Johnson kuwa anampenda kutokana na sababu mbili, kwanza ingekua si maadili mema kutokana na utamaduni wao, pia Mary alikua binti aliyekua amekuzwa kwenye maadili ya dini sana. Lakini mapenzi hayajifichi , Mary alianza kumuonyesha matendo  na vituko vya hapa na pale ilimradi tu aeleweke kwa Johson.
Kila binadam anautashi wa kutosha, hatimae Johson akamuelewa Mary, na wakajikuta wameanzia urafiki wa awali na kwa kuanzia wakapeana namba za simu wakawa wakiwasiliana.

Mary alikua binti aliyekuzwa katika maadili ya kidini, na alikua binti wa kawaida mcheshi mwenye heshima na maadili, alikua binti mnene wa wastani, mfupi kiasi , mweusi wa asili, alikua akikata nywele zake mda wote. Licha ya haiba hiyo. Mary alikua mchapa kazi na binti aliyejituma sana, licha ya kuajiriwa na Mgahawa wa Chichechi City Garden, alikua anamiliki duka la bidhaa za nyumbani, Kwa wakati huo alikua akiishi Doro, chini kidogo ya mji wa Kithinthua. Pia alikua mwimbaji mzuri wa kwaya kanisani kwao.

ADAMSON & EVACENCIA-1



ADAMSON & EVACENCIA!

Nilifumbua macho nikaanza kuangaza huku na huko, wala haikuwa na aja ya kupata maelezo ilikua ni mazingira ya hospitali, mandhari ilionyesha tu hivyo, nikajiuliza nimefikaje hapa na ni ugonjwa gani umesababisha nimefika hapa, nilianza kujiuliza bila kupata majibu, sikukumbuka kama kabla nilishikwa na ugonjwa wowote, wakati huo dribu niliyokua nimetundikiwa ilikua imebaki kama robo chupa iweze kuisha, ghafla niliona mlango wa chumba nilichokua ukifunguliwa akaingia nesi, alikuwa akitabasamu akaja karibu kabisa na kitanda nilichokua nimelala akaniinamia kasha kwa sauti ya upole akaniambia ‘’pole dada unajiskiaje kwasasa?’’ nikamjibu ‘’ahsante nesi’’ akaniambia anaitwa nesi Annastazia, akaniambia nipo ST.Mary Hospital, uliletwa hapa ukiwa umepoteza fahamu, unaweza kukumbuka chochote kilicho kupata mpaka hali ikawa hivi? Waliokuleta walisema ulikua H & G Hotel wakakuona kama umepatwa na mshtuko na ukapoteza fahamu, ndio wakakukimbiza hapa, baada ya nesi Anastazia kuyasema hayo nikajikuta nikisema Adamson Adamson Adamson, nilitamka jina hili kwa kigugumizi na kuweweseka hatimae nikaona giza likiingia machoni hatimae nikazimika! Nilipozinduka kwa mara nyingine tena walas sikuhitaji maelezo yoyote yakunikumbusha nini kilichotoke kabla ya kufikishwa hapa, nilianza kukumbuka kilichotokea mchana wa siku hiyo, nilikua H & G Hotel, hotel ambayo tulipendelea sana kukutana na mpenzi wangu Adamson, na kukumbuka ilikua siku ya jumamosi nilifika hotelini majira ya saa nane na nusu kwa miadi ya kukutana na mpenzi wangu huyo ambaye alikua bado yupo kazini, Hoteli ilikua na ghorofa nne na ghorofa ya nne ndio kulikua na huduma ya mgahawa, nilifika kwenye meza moja iliyokua karibu kabisa na dirisha ambapo ningeweza kuona mandhari kubwa ya mji pia barabara na sijui ni kwanini nilihisi mpenzi wangu angetokea upande huo. Ingawa nilikua sijaonana nae kwa siku moja tu nilihisi kummisi sana, hakika tulipendana ukizingatia majina yenyewe ndio hivyo tena yeye Adamson na mimi Evacencia, au Eva.

***
Nikiwa nipo kwenye lindi la mawazo kwa mbali nikamuona mahabuba wangu akitokeza upande wapili wa barabara alikua akija kwa mikogo, kweli kutokea kwenye mwendo wake niligundua hata yeye alikua amenimisi, alikua akitembea kwa haraka lakini kwa mikogo huku akiwa ameweka headphone, sijui hata alikua akisikiliza mziki gani, mwanaume alinimaliza huyuu!! Hata sijui aliniloga na nini?, sio siri nampenda sana na naamini hata yeye ananipenda sana, ghafla alikua anavuka barabara nikiwa nimetingwa kumuangalia likatokea gari lililotoka na kumvamia mpenzi wangu, kwakweli sikumbuki kilichoendelea kwani nilipatwa na mshtuko mkubwa, nikapatwa na giza machoni baadae nikazimika kabisa. Nilipokua naendelea kukumbuka hayo nikamuona nesi Anastazia akiingiia

KISIMA CHA MATATIZO-1

KISIMA CHA MATATIZO:

SURA YA KWANZA:
‘’Nikweli najua ipo siku nitasahau shida zangu zote, lakini kwasasa naona giza sijui namna ya kutatua matatizo niliyonayo!’’ mbaya zaidi kila likiisha moja linaanza jingine, sijui ni mkosi au laana’’ ilikua ni sauti ndogo yenye mvuto lakini ilitoka kwa kukata kata toka kwenye midomo mipana yenye mvuto, kwasasa urembo wake ulikua umejificha kutokana na simanzi na machozi yaliyokua yakitiririka mashavuni mwa binti huyu, Alikua akiitwa Pamela, lakini wengi walifupisha jina lake na kumuita Pam, Alikua ameketi kwenye kochi moja lililokua chumbani humo, kwenye kochi la jirani yake ailikua amekaa Mary, mary alikua rafiki yake na Pamela toka wakiwa shule ya msingi. Chumba hiki walichokua wamekaa Pamela na Mary, ilikua ni nyumbani kwa akina Mary aliyekuwa akiishi na dada yake na shemeji yake.

*****

Lucy alikua ni motto wa pekee toka kwenye familia ya Mzee Peter Mihambo, wa mjini Mwanza maeneo ya Magu, Mzee Peter alikua ni Mzee mwenye uwezo kijijini na pia alikua na elimu ya kutosha kwa wakati huu alikua amestaafu  lakini alikua akimiliki mifugo pia alikua akimiliki boti ndogo kwa ajili ya shughuli za uvuvi Ziwa Victoria, hayo yote yalimpa heshima pale kijijini, wazee wenzie walikua wakimuita Mzee PETERI.
Kwa wakati huo Lucy alikua darasa la sita katika shule ya msingi magu. Lucy alikua na maendeleo mazuri sana shuleni toka akiwa darasa la kwanza, pia alikua ni motto mwenye tabia nzuri jambo lililompa heshima pia Mzee Peter, Mzee Peter mara kwa mara alimweleza binti yake ata hakikisha amemsomesha mpaka ngazi ya juu ya elimu, hata kama itamlazimu kuuza mifugo yake yote. Ingawa Lucy alikua darasa la sita  tu wakati huo lakiniuzuri na urembo wake haukujificha, Lucy alikua mzuri wa sura na hata umbo lake lilifinyangika vizuri na rangi yake ya maji ya kunde iliongeza chachu zaidi, kama yangefanyika mashindano ya ulimbwende basi Lucy angenyakua taji bila mjadala.

Kama ilivyokua kwa Mzee Peter, mama mzazi wa Lucy Bi. Imelda hakua nyuma katika kumpa malezi bora binti yao Lucy, na hata ilipobidi kuwa mkali alikua mkali ili tu binti yao asije kuingia kwenye vishawishi vya ulimwengu huu. Na kwa wakati huo tatizo la kijijini pale ilikua mabinti wengi kushindwa kumaliza shule au kumaliza wakiwa wajawazito. Mzee Peter pia alikua mkali kwa binti yake juu ya swala hilo, alikua akimweleza binti yake kua kama atamuaibisha kwa swala hilo basi atahakikisha anamtenganisha kichwa na kiwili wili.

SURA YA PILI:
Wataalam wa mambo wanasema karibu wanawake wote hawana ‘’wazo la pili’’ (second thought). Kwa bahati mbaya sana, Hata Lucy alijikuta akiingia kwenye kundi hili la wasio kua na wazo la pili. Alikua darasa la saba akajikuta ameshawishika na kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wake wa darasa kwa ahadi kua atamuuibia mtihani wa mwisho wa kuhitimu darasa la saba. Lucy kwa wakti huo alifikiri juu ya kuibiwa tu mtihani akasahau kuwaza kuhusu madhara ya uhusiano huo wa kimapenzi.
Lucy aliendelea na uhusiano huo wa kimapenzi na mwalimu wake wa daras, Mwalimu Dennis, bila mtu yeyote kugundua . ilikua ngumu sana kugundulika kwani Lucy alikua karibu sana na walimu wake karibu wote tofauti na wanafunzi wengine walio kua wakiwaogopa walimu. Siku zote za mwizi ni arobaini, miezi miwili kabla hajaitimu elimu yake ya shule ya msingi, walikuja wageni shuleni kwao kutokea wizara ya afya, ugeni huo uliendesha zoezi la kuwapima ujauzito wanafunzi wote wa kike wa darasa la saba, ndipo ilipogundulika wanafunzi ishirini wanaujauzito akiwemo Lucy, aliyekua na ujauzito wa mwenzi mmoja. Taarifa zilifika nyumbani kwa akina Lucy, kwa bahati baba yake na Lucy hakuwepo nyumbani, alikua amekwenda kisiwani ukerwe kwa shughuli za uvuvi, hivyo taariza za ujauzito zilimfikia mama yake Lucy bi. Imelda. Mama yake Lucy alipatwa na simanzi sana, lakini siku zote motto kwa mama hakui, nawahenga walisema Mtoto akinyea kiganja huwezi kukikata. Bi Imelda alimuonea huruma binti yake, akamuuliza mhusika wa ujauzito huo ni nani. Lucy bila kumficha mama yake akamueleza ukweli wote, mama yake alimpa pole kasha akamuuliza lakini mwanangu unakumbuka baba yako alikua akikueleza nini kuhusu swala hili endapo litatokea,? Lucy hakuweza kujibu alivuta pumzi na kujiinamia kabla ya kuangua kilio kikubwa kilichoaambatana na kwikwi, Lucy alikua akijuta lakini siku zote majuto ni mjukuu, Lucy alilia kwa mambo mawili kama sio matatu, la kwanza ilikua kukatiza masomo yake, lapili ilikua mhusika wa ujauzito huo, mwalimu denis alikutwa amejinyonga chumbani kwake kuhofia mkono wa sheria na la tatu ilikua ni hatua ambayo baba yake angechukua mara baada ya kurejea. Bi Imelda alinyanyuka alipokua mekaa akamfuata mwanae, akamsogelea akaanz kumfuta machozi, akamwambia nyamaza binti yangu, maji yakisha mwagika hayazoleki, naomba unyamze na usikilize kwa makini sana, akaanza kuongea huku amemkazia macho kidogo binti yake akamwabia ‘’ namfahaamu mzee mihambo akisema jambo lake, amesema’’ hivyo mwanangu kuna wazo limenijia kichwani itabidi nikutoroshe mpaka pale baba yako hasira zitakapopungua, kuna akiba yangu iliyokua nimehifadhi itabidi nikupatie kesho asubuhi nikutoroshe uende dar, ukamtafute mama yako mdogo atakusaidia, kinyume na hivyo baba yako akikukuta hapa atakuua kweli. Bi Imelda alimkumbatia mwanae akamwambia ajiandae kwasafari alfajiri iliyofuata kwani usiku ulikua umeshaingia. Kwa kweli usiku huo haukua mzuri sana kwa Lucy, alilala usingizi wa mangam ngam na mara nyingine kuota ndoto za kutisha tisha, Hauchi hauchi, unakucha hatimae alfajiri ilifika, bi Imelda alimtorosha bintie, bila watu kumuona na Lucy akapanda treni kuianza safari yakuelekea dar, njiani alionekana mwenye mawazo sana na wakati mwingine alijisahau na kuanza kulia kabisa,

******
Jioni ya siku hiyo hiyo aliyotoroshwa Lucy, ndio mzee mihambo alirejea nyumbani akitokea ukerewe kwenye shughuli zake za uvuvi. Tofauti na siku zote nyingine alizokua akipata mapokezi bashasha toka kwa mke wake kipenzi kila lipotoka safari, hata kama ingekua safari fupi, siku hiyo hakupata mapokezi yeyote toka kwa mkewe. Bi Imelda alikua amejiinamia mbele ya nyumba yao, huku akionekana mtu mwenye masikitiko na majonzi, hukua akionekana mtu aliyeshinda akilia, Bi Imelda alipomuona mume wake, alijizoa zoa kutoka mahala alipokua amekaa na kumpoke mumewe, Mzee Mihambo kabla ya kuingi ndani ya nyumba aligundua mambo hayakua shwari nyumbani kwake. Mzee Mihambo alimuuliza mkewe ‘’ kuna usalama kweli hapa mke wangu?’’ Bi Imelda hakuweza kuongea chochote, zaidi ya kutokwa na machozi, ndipo alipojikaza na kumjibu mumewe. Kua aingie ndani kwanza, aoge na kupumzika kwanza ndipo atamueleza yaliyojiri akiwa safarini. Baada yam zee Mihambo kuoga na kupumzika ndipo alipokaa na mkewe, Bi Imelda alimueleza mumewe yote yalijiri kwa kipindi hicho ambacho hakuwepo nyumbani na alipofika kwenye mada ya ujauzito wa Lucy, alijikuta akilengwa lengwa na machozi, akavuta pumzi kasha akazishusha akaendelea kumueleza mumewe kua kilichomsikitisha zaidi kuwa Lucy ametoroka na hajui amekwenda wapi ( alimdanganya mumewe) mzee mihambo aliinamisha kichwa chini kwa muda, na alipokinyanyua alikua amebadilika, uso wake ulionyesha hasira na dhahiri macho yake yalikua mekundu, ndipo akamwangalia mkewe kwa macho makali na kumwambia kua, yeye ndiye anayejua siri yote ya binti yake, akamwambia atagundua ukweli wote na kusema kua afadhali amemtorosha binti yake mapema,  maana kama angemkuta ingekua ndio mwisho wa maisha yake. Baada ya kuyasema hayo, Mzee Mihambo alinyanyuka na kuondoka kwa hasira. Bi Imelda alibaki aikwa amejiinamia huku akilia kwa kwikwi.

*******
Ilikua ni ndani ya treni, masaa yalikua yamesogea sana toka treni hiyo ilipo acha viunga vya stesheni mjini Mwanza. Abiria walikua wakiendelea na shughuli mablimbali wengine walionekana wakipiga hadithi za hapa na pale wengine midomo ilionekana ikitafuna na wengine walikua wamesinzia, Kwenye Treni hiyo ndipo alipokuwemo Binti Lucy, tokea safari ilipoanza mjini mwanza, alionekana akiwa mwenye mawazo mengi sana, pembeni yake alikua ameketi dada wa makamo kidogo, dada huyo alionekana kumfuatilia Lucy toka safari ilipoanza, Dada huyo aliamua kuvunja ukimya, akamuuliza ‘’samahani mdogo wangu mbona unaonekana mwenye mawazo sana, natoka safari ianze sijakuona ukila chochote?’’ Lucy hakuweza kujibu chochote zaidi ya kutiririkwa na machozi, dada Yule hakuchoka kumwambia ‘’Pole dada unaonekana unamatatizo, samahani kama nakukwaza mimi naitwa dada Patricia, ingawa wengi wananiita Sia, ni mfanya biashara, naishi dar, maeneo ya magomeni mwembechai’’ ndipo Patricia alipotoa keki mbili na kumpatia Lucy akimwambia apooze njaa, Lucy alimshukuru dada Yule kwa ukarimu wake. Lucy alijitambulisha kwa Patricia kua yeye alikua akiitwa Lucy. Na ni motto yatima, na pale mwanza alikua akifanya kazi za ndani, ndipo alipobakwa na kupewa ujauzito (Alimdanganya) hivyo anakwenda jijini dar kumtafta mama yake mdogo aliyekua akiishi maeneo ya manzese, Lucy alitoa picha aliyopewa na mama yake ikiwa na sura ya mama yake mdogo huyo, aliyemwambia Patricia kua alikua akiitwa Daniella. Patricia aliangalia picha ile kasha akamgeukia Lucy, akamwambia ‘’Pole sana mdogo wangu kwa yote, lakini kwa jiji kubwa kama dar kumtafuta ndugu yako kama huyo itakua ngumu, ila usijali nina rafiki yangu anayeishi maeneo ya manzese hivyo basi tutakapofika dar, nitakupeleka kwa rafiki yangu huyo, umsaidie kwenye biashara yake ukiwa unaendelea kumtafuta mama yako mdogo. “ Lucy alifurahishwa na hatua hiyo akamshukuru Patricia’’

SURA YA TATU:
Ilikua ni taarifa ya habari ya saa nne asubuhi, ndipo mtangazaji aliporipoti tukio la kusikitisha lililotokea mjini mwanza usiku wa kuamkia siku hiyo. Mtangazajia aliripoti kua familia moja mjini mwanza, maeneo ya Magu wamekutwa wameuwawa kufuatia kuchomwa moto nyumba yao na mifugo yao na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na uchunguzi zaidi unaendelea, kujua ukweli wa tukio hilo la kinyama. Mtangazaji aliporipoti kua watu waliouwawa ni Mzee Peter Mihambo na mkewe bi Imelda mihambo. Wakati huo Lucy na Patricia walikua tayari wako kwenye daladala lililokua likitokea stesheni kuelekea ubungo, jijini dar, wakati taarifa ya habari hiyo ikiendelea ndipo Lucy alipoangua kilio, Patricia akamuuliza Lucy ‘’Vipi unawafahamu au?’’ Lucy hakuweza kujibu chochote, kwasababu alishamdanganya kPatricia kua yeye alikua motto yatima, ingawa taarifa hiyo ilimuuma sana mpaka bado kidogo aseme ukweli, lakini kwa wakati huo hakua na kitu chakufanya, kondakta wa gari hiyo aligonga akauliza kama kuna mtu aliyekua akishuka manzese, ndipo Patricia alipomshtua Lucy kua wamefika hivyo wateremke, Lucy alikua ameishiwa nguvu kabisa lakini alijikaza, wakateremka kutoka kwenye gari hiyo. Patricia alimuongoza Lucy na kuingia mitaa kadhaa iliyokua ndani ndani ya manzese kabla hawajakaribia nyumba moja chakavu kidogo iliyokua na vibanda viwili vya mabati machakavu kidogo pia. Patricia akamwambia ‘’tunapokwenda ndio pale, tumeshafika, futa basi hayo machozi’’ Lucy akawa ni kama mtu aliyetoka usingizini, baada ya kuyasikia maneno hayo toka kwa Patricia! Maana alikuwepo kimwili tu, mawazo yake yote hayakua pale, yalikua kwa wazazi wake mwanza na kichwani mwake aliisikia ile sauti ya mtangazaji ikiripoti tukio la mauaji ya wazazi wake ikijirudia rudia. Hawakupiga hata hatua tano wakawa wamesimama mbele ya nyumba ile, Patricia akatangulia ‘’Hodi Hodi Shoga yangu’’ sauti ikajibu ‘’Karibu shoga yangu Sia’’, Kutokea kwenye kibanda cha upande wa kulia akatoka dada wa makamo kidogo kama Patricia akawakaribisha ‘’Karibuni ndani, naona ndio mwaingia, namalizia kumpimia mteja supu naja.’’ Patricia akamuongoza Lucy kuingia ndani ya nyumba hiyo ingawa ilikua asubuhi lakini ndani humo kulikua na giza kutokana na madirisha ya nyumba hiyo kua madogo. Patricia akamkaribisha Lucy kwenye kochi lilikoua ndani humo ‘’Karibu mwaya uketi, ndio dar hii, hapa ndio utakapokua unaishi, ndio kwa Yule rafiki yangu anayeitwa Rehema, anaroho nzuri tu, hivyo najua mtaishi vizuri tu, au sio mdogo wangu Lucy?’’ Lucy akajibu ‘’ ndio dada yangu’’ zilipita kama dakika tatu za ukimya ndipo Rehema akaingia ndani humo na kuvunja ukimya huo ‘’Habari za safari jamani?’’ ‘’nzuri. Sijui za huku kwenu?’’ ‘’Ahaaa!! Njema, kama unavyotuona, tunaganga ganga’’ ‘’sasa rafiki yangu rehema bila ya kupoteza mda, huyu anaitwa lucy, nimekutana nae kwenye treni-mwanza, akanieleza matatizo yake, nikaona nije nae hapa akusaidie shughuli zako, akiwa anamtafta mama yake mdogo, hiyo nikwa ufupi tu, mengi zaidi atakueleza mwenyewe au wewe unaonaje?’’ ‘’kweli!!, Lucy karibu mwaya, jisikie upo nyumbani, tutasaidiana kwa kila hali, matatizo ni sehemu ya maisha mdogo wangu’’ Lucy aliwashukuru wote kwa pamoja, Patricia nae hakukaa sana akawaaga na kuondoka. Basi ukawa mwanzo wa maisha mapya ya Lucy jijini dar, akawa akimsaidia rehema kuuza supu na pombe katika vilabu vyake, rehema alikua na moyo mzuri, alimchukulia Lucy kama mdogo wake kabisa, taratibu taratibu kadri siku zilivyokua zikisogea, Lucy akajikuta akisahau mambo ya Mwanza na kuzoea dar, na pia kuzoea hali yake ya ujauzito. Kiufupi aliamua kumuachia Mungu mambo yake yote, hali hiyo ilimfanya Lucy anawiri na uzuri wake uonekana dhahiri. Lucy akaanza kupata vishawishi vya hapa na pale kutoka kwa wanaume waliokuwa wanakuja kama wateja na hata ambao hawakua wateja. Lakini Lucy alikua na msimamo mpya hakua anataka mwanaume yeyote amshawishi wala kumchezea mwili wake, na kwakiasi Fulani aliweza kuwadhibiti, kwani wanaume wote waligonga ukuta.

*****
Nilihisi kama umeme fulaniukinitembelea mwilini, pale aliponikumbatia kwa nyuma, maneno yake yalitetemesha ngoma za masikio nyangu pale aliposema ‘’Hivi ni kweli Lucy hunipendi?’’ hebu niangalie usoni na uniambie hunipendi’’  Nilijibaraguza nkamgeukia badala ya kufuata alichonieleza, nikamwambia kwa aibu aibu huku nikikwepesha macho ‘’Hivi Andrwe nani alikupa idhini ya kunikumbatia?’’  Kwa mara ya kwanza nilihisi nikimpenda Andrwe. Mwanaume ni Mwanaume tu, alipuuza niliyomwambia akanishika mkono tukaketi kwenye Bechi moja lililokuwepo kibandani mle, kulikua hakuna wateja. Kwa sauti ya ukakamavu na kujiamini akaniambia ‘’Sijui kwa nini huniamini Lucy,’’Mimi nipo tofauti sana na hawa wanaume wengine wa hapa, Lengo langu sio kukuchezea au kukutumia kwa starehe za muda mfupi, lengo langu nahitaji tuanze kuishi pamoja kama mume na mke, nielewe Lucy nakupenda’’ alipofikia hapo aliongea kwa masikitiko zaidi huku akiniangalia machoni,  kwa aibu za kike nikainamisha kichwa chinihuku niking’ata kucha,nikaanza kumjibu kike kike,nikamwambia itakua ngumu kwanza ni mdogo alafu ninaujauzito utakubali vipi kule  ujauzito na mototo ambaye sio wako, alafu hapa DSM sina ndugu yoyote, Dada Rehema ndio kila kitu kwangu kwa hio itakuwa ngumu.Baada yakuyasema hayo nikajua atasimama na kuondoka lakini badala yake, Akaniambia ‘’Sikiliza Lucy mimi nakupenda sana na waswahili  walisema ukipenda Boga upende na Ua lake hivyo wala usitilie shaka kuhusu ujauzito na mengine yote Patrisia ameshanieleza ‘’ Nikashtuka kidogo nikamwambia na Patrisia unamfahamu? Akajibu ‘’Ndio’’ akaendelea akaniambia ‘’Kwa hio Lucy swala lipo kwako kama wewe umekubali basi mwambie dada yako Rehema atakachosema utanieleza’’ sawa?’’ Kabla sijajibu  Dada Rehema akatokea Eeeh Andrwe hujaenda tu,au umeniletea kreti jingine la  bia, la ofa, iwe heri tu hapo na mdogo wangu,  maana nyie wanaume msione’’ Andrwe hakusema kitu zaidi ya kutabasamu na kuondoka zake.

******

Siku hio Lucy alishinda akiwa na furaha kweli hata kazi zake siku hio alizimaliza mapema kweli, ukweli ni kwamba hata yeye alihisi kumpenda Andrwe. Usiku akiwa anajiandaa kulala, akaona ni vyema amueleze dada yake Rehema, Basi Lucyakaamua kumueliza ukweli wote Rehema. Rehema akamwambia Lucy ‘’Sikiliza Lucy wanaume hawaaminiki, lakini huwenda hii ikawandio bahati yako.’’ Kwa jinsi mimi ninavyomfahamu Andrwe sio mtu mbaya labda abadilike, hivyo basi kama wewe mwenyewe umeridhia basi mkubalie ombi lake, Kama utaenda huko na yatakushinda basi jirudie hapa sasa ni kama nyumbani kwako,  hivyo tuombe heri tu. Lucy alifurahishwa sana na maneno hayo, wote wakatakiana heri ya usiku mwema na wakalala.
Baada ya majuma mawili kupita, Lucy alihamia rasmi nyumbani kwa Andrwe, Lucy alishangaa sana alipofika nyumbani kwa Andrwe, Andrwe alikua amejitahidi sana kimaisha, Ingawa alikua amepangisha chumba kimoja tu, lakini kilikua kikubwa na kilikua kinavitu vyote ambavyo mwanaume anayeanza maisha anatakiwa awe navyo. Kulikua na kitanda kikubwa cha 5 kwa 6, kabati la nguo, makochi, kabati la vyombo, meza, stuli, Redio kubwa, na friji ngodo huku sakafuni kukiwa na zulia matata [kipindi kile TV zilikua hazijaenea sana lakini huenda angekua nayo] Hivyo vyotevilimchanganya sana Lucy, Lucy akamuuliza Andrwe’’ Vijana wote hapa Magomeni ni matajiri kama wewe au?’’ Andrwe akamuuliza kwa nini? Si vitu vyote vya thamani sikutegemea! Andrwe akamjibu akamwambia ni uaminifu tu ndo ulinifanya niwe hivi, Huyu Bosi wangu nilianza kazi kwenye baa yake kama weita tu lakini kwa sababu ya uaminifu ndio maana ameniachia nisimamie kabisa baa yake pamoja na kusambaza vinywaji sehemu mbalimbali kama ilivyokua pale kwenu. Lucy alimpongeza sana Andrwe na Andrwe akamkaribisha Lucy hapo rasmi kama mke wake. Ikawa mwanzo mwingine mpya na mzuri kwa Lucy.


                                            SURA YA NNE
Ikawa imepita miaka 15 toka Andrwe na Lucy waanze kuishi pamoja, kwa sasa hawakua wawili tena bali walikua familia, Lucy alikua sio Lucy tena alikua akiitwa mama Pamela, Ilikua familia yenye furaha na maendeleo, walikua bado wakiishi Magomeni. Andrwe alikua kichwa imara cha familia hiyo kwani ndani ya miaka 15 hiyo familia ilikua imejaa furaha na Amani, pia Andrwe alipanga kumpatia mkewe  kazi  kwenye baa ile aliyokuwa akifanyia kazi,pia alikuwa akimsomesha Pamela na kwa sasa Pamela alikua kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Jangwani. Pamela alikua binti mzuri na mwenye tabia njema na bidii katika masomo, mara nyingi alikuwepo nyumbani na kama usipomkuta ametumwa au anajisomea kwa rafiki yake Mary alikua akiishi mtaa wa pili toka kwa akina Pamela, Mary alikua rafiki kipenzi wa Pamela,walikuwa wakisoma wote shuleni Jangwani. Mary alikua akiishi na dada yake n shemeji yake.
Licha ya familia ya kina Pamela kuwa na faraha lakini kulikua na matatizo macchache ambayo wakati fulani yangeweza kufanya furaha hiyo iyeyuke na kuleta majonzi kwa wahusika. Lucy toka alipomzaa Pamela hakuweza kubeba ujauzito tena na baadhi ya madaktari kuwaLucy asingeweza kubeba ujauzito tena. Hilolilikua tatizo kati ya Andrwe na Lucy, lakini ukiacha hilo, Luch ni mara nyingi sana alisongwa na msongo wa mawazo,swala lililokua linamtatiza kwambaamwambie au asimwambie au aendelee kumficha mpaka lini Pamela kuwa Andrwe sio baba yake mzazi. Maswala haya kwa namna moja au nyingine yalikuwa yakiitatiza familia hii.

*****
Ilianza kama utani, ilikua ni jioni moja Lucy akiwa ametoka kazini, alianwa na maumivu ya tumbo yaliyokua makali sana,kiasi kwamba machozi yalikua yakimtoka,Pamele alikua kasharudi pia kutoka shuleni na alikua akiishuhudia hali ya mama yake, Alivyoona inazidi kua mbayaaliona ni bora amfuate baba yake kazini ili wampelrke mama hospitali, Andrwe aliofika nyumbani alishangaa sana kumkuta mke wake akiwa kwenyw hali ya maumivu makali wakati mda mfupi tu umepita alikua kazini mzima kabisa. Ikambidi tax nakumkimbiza zahanati iliokua karibu na mtaani kwao, walipofika Lucy aliingizwa moja kwa moja daktari. Kutokana na hali aliyokua nayo ilibidi aandikiwe kulazwa. Ilibidi Pamela na baba yake warudi nyumbani.