Wednesday, February 13, 2013

ADAMSON & EVACENCIA-1



ADAMSON & EVACENCIA!

Nilifumbua macho nikaanza kuangaza huku na huko, wala haikuwa na aja ya kupata maelezo ilikua ni mazingira ya hospitali, mandhari ilionyesha tu hivyo, nikajiuliza nimefikaje hapa na ni ugonjwa gani umesababisha nimefika hapa, nilianza kujiuliza bila kupata majibu, sikukumbuka kama kabla nilishikwa na ugonjwa wowote, wakati huo dribu niliyokua nimetundikiwa ilikua imebaki kama robo chupa iweze kuisha, ghafla niliona mlango wa chumba nilichokua ukifunguliwa akaingia nesi, alikuwa akitabasamu akaja karibu kabisa na kitanda nilichokua nimelala akaniinamia kasha kwa sauti ya upole akaniambia ‘’pole dada unajiskiaje kwasasa?’’ nikamjibu ‘’ahsante nesi’’ akaniambia anaitwa nesi Annastazia, akaniambia nipo ST.Mary Hospital, uliletwa hapa ukiwa umepoteza fahamu, unaweza kukumbuka chochote kilicho kupata mpaka hali ikawa hivi? Waliokuleta walisema ulikua H & G Hotel wakakuona kama umepatwa na mshtuko na ukapoteza fahamu, ndio wakakukimbiza hapa, baada ya nesi Anastazia kuyasema hayo nikajikuta nikisema Adamson Adamson Adamson, nilitamka jina hili kwa kigugumizi na kuweweseka hatimae nikaona giza likiingia machoni hatimae nikazimika! Nilipozinduka kwa mara nyingine tena walas sikuhitaji maelezo yoyote yakunikumbusha nini kilichotoke kabla ya kufikishwa hapa, nilianza kukumbuka kilichotokea mchana wa siku hiyo, nilikua H & G Hotel, hotel ambayo tulipendelea sana kukutana na mpenzi wangu Adamson, na kukumbuka ilikua siku ya jumamosi nilifika hotelini majira ya saa nane na nusu kwa miadi ya kukutana na mpenzi wangu huyo ambaye alikua bado yupo kazini, Hoteli ilikua na ghorofa nne na ghorofa ya nne ndio kulikua na huduma ya mgahawa, nilifika kwenye meza moja iliyokua karibu kabisa na dirisha ambapo ningeweza kuona mandhari kubwa ya mji pia barabara na sijui ni kwanini nilihisi mpenzi wangu angetokea upande huo. Ingawa nilikua sijaonana nae kwa siku moja tu nilihisi kummisi sana, hakika tulipendana ukizingatia majina yenyewe ndio hivyo tena yeye Adamson na mimi Evacencia, au Eva.

***
Nikiwa nipo kwenye lindi la mawazo kwa mbali nikamuona mahabuba wangu akitokeza upande wapili wa barabara alikua akija kwa mikogo, kweli kutokea kwenye mwendo wake niligundua hata yeye alikua amenimisi, alikua akitembea kwa haraka lakini kwa mikogo huku akiwa ameweka headphone, sijui hata alikua akisikiliza mziki gani, mwanaume alinimaliza huyuu!! Hata sijui aliniloga na nini?, sio siri nampenda sana na naamini hata yeye ananipenda sana, ghafla alikua anavuka barabara nikiwa nimetingwa kumuangalia likatokea gari lililotoka na kumvamia mpenzi wangu, kwakweli sikumbuki kilichoendelea kwani nilipatwa na mshtuko mkubwa, nikapatwa na giza machoni baadae nikazimika kabisa. Nilipokua naendelea kukumbuka hayo nikamuona nesi Anastazia akiingiia

1 comment:

  1. Tabletop Safety Razor - titanium fitness
    One of the best selling safety razors of the era is the Silver Dragon. titanium fishing pliers It is constructed with an titanium joes aluminium alloy and can be attached titanium rod in leg to the titanium piercing jewelry top of the titanium dive watch razor

    ReplyDelete