Wednesday, February 13, 2013

ZAWADI YA SANDA-1



ZAWADI YA SANDA.

Bado ni giza x 2, sioni wapi pakupapasa naishangaa sayari hi…’’ ulikua ni wimbo uliokua ukisikika toka chumbani kwa kijana Johnson kwa wafuatiliaji wa muziki watakua wameshajua wimbo huu ni wa nani, si mwingine ni kijana Matonyaaliyekua akivuma kipindi hicho, Hakika ilikua Tonya time. Licha ya wimbo huu kusikika kwa sauti ya juu, lakini wala kijana Johnson hakuwa akiusikia, kiganja chake kilikua bize kikichezea simu yake ndogon ya kiganjani na alikua amezama kwenye lindi zito la mawazo si kwakua alikua bize na simu la hasha! Kwani hata alichokua akikifanya kwenye simu hakukielewa, kiukweli akili yake ilikua haijatulia kabisa, Alikua ameketi kwenye sofa iliyokua chumbani humo, mbele yake sakafuni kulikuwa na mwili wa mwanamke ukiwa umelala haujitambui. Harufu ya kifo ilikua ikinukia!!! Akili ya Johson ilifanya kazi haraka sana, akaamua kumpigia simu rafiki yake David waliyekua wakiishi nae kwenye kota hizi za kupangisha maeneo ya Ntana, katika mji wa Kithithua. Siku ya kufa nyani miti yote huteleza alijisemea Johnson, pale alipokua amempigia simu David mara kadhaa lakini simu haikupokelewa, Johson alizidi kuchanganyikiwa kwani pia haikua kawaida ya David kuchelewa kurudi hadi usiku huo, Aliamua kujaribu kwa mara nyingine kuipiga simu hiyo ya swaiba yake! Kama mara kadhaa zilizopita simu hiyo iliita tu pila kupokelewa, mara nyingine tena akajaribu ikaitaa kwa muda mrefu lakini kabla haijakatika ikapokelewa upande wa pili…!

*****
Ulikua ni mgahawa mkubwa uliokusanya watu mbali mbali wa mjini pale, kutokana na kua katikati ya mji wa Kithinthua na pia bei za mgahawa ule zilikua ni za wastani hivyo kila mtu wa kuanzia kipato cha wastani aliweza kumudu kuingia mgahawani pale palipokua pia panaongoza kwa huduma na chakula kizuri kilichosifiwa na wengi, ndipo hapa Johson alipokutana na mwanadada Mary Limuli aliyekua mhudumu wa mgahawa huu wa Chichechi City Garden, ilianza kama utani kwa wawili hawa kuzoeana na hatimae kutumbukia kwenye dimbwi la mahaba mazito.

Johson alikua ni mwalimu katika chuo kimoja maarufu mjini Kithinthua, kilichojulikana kama Ville Technology College. Johnson alikua kijana mtanashati, mchapa kazi na mtu wa kujituma sana, ingawa walio wengi walikua wakisema Johnson alikua akiringa lakini ukweli alikua akionekana tu hivyo lakini sio uhalisia wake kwani alikua hana majivuno, mtu wa utani na mizaha ingawa hili usingeweza kulitambua mpaka umemzoea na kukaa nae kwa mda kidogo, wahenga walisema kizuri hakikosi kasoro ndivyo alivyokua pia Johson kwani kasoro yake kubwa ilikua ni kupenda wanawake, vijana wanasema alikua mzee wa totoz!! Ni tabia hii iliyokuja kumuingiza matatizoniingawa mwenyewe alikua akijigamba kua alikua mzee wa mapenzi ya kigumu, au Gengstar Loving kwa lugha ya wamarekani weusi, Wanawake wake wengi alikua akienda nao kula kwenye mgahawa wa Cichechi City Garden, kitu alichokua akikifanya bila kujua kua alikua akimuumiza Mary, Mary alikua amempenda Johson toka siku ya kwanza alipomuona, lakini ilikua ngumu kumueleza ukweli, aliishia kumtania tu,
Ilikua ngumu kwa Mary kumueleza Johnson kuwa anampenda kutokana na sababu mbili, kwanza ingekua si maadili mema kutokana na utamaduni wao, pia Mary alikua binti aliyekua amekuzwa kwenye maadili ya dini sana. Lakini mapenzi hayajifichi , Mary alianza kumuonyesha matendo  na vituko vya hapa na pale ilimradi tu aeleweke kwa Johson.
Kila binadam anautashi wa kutosha, hatimae Johson akamuelewa Mary, na wakajikuta wameanzia urafiki wa awali na kwa kuanzia wakapeana namba za simu wakawa wakiwasiliana.

Mary alikua binti aliyekuzwa katika maadili ya kidini, na alikua binti wa kawaida mcheshi mwenye heshima na maadili, alikua binti mnene wa wastani, mfupi kiasi , mweusi wa asili, alikua akikata nywele zake mda wote. Licha ya haiba hiyo. Mary alikua mchapa kazi na binti aliyejituma sana, licha ya kuajiriwa na Mgahawa wa Chichechi City Garden, alikua anamiliki duka la bidhaa za nyumbani, Kwa wakati huo alikua akiishi Doro, chini kidogo ya mji wa Kithinthua. Pia alikua mwimbaji mzuri wa kwaya kanisani kwao.

No comments:

Post a Comment