Mapishi ya keki
Siku zote mtu anatakiwa awe mbunifu kwa kila kitu.Ila leo nagusia upande wa jikoni.Kwa upande wa wanawake katika sekta nzima ya maakuli mambo ya jikoni shuti unatakiwa uwe mtundu,leo unabuni hiki na kesho unafanya vile ili mradi uweze kupata vionyo tofauti tofauti.Raha ya chakula shuti upike mwenyewe bibi..'mwanamke jiko eeh''.Kwa wale wanawake wafanyakazi,siku ukiwa nyumbani umejipumzisha na laazizi wako unaamua umuandalie kitu tofauti ambacho kitamfrahisha nae aone kuwa mama watoto wake anajua kulikalia jiko na si kila siku anakula chakula alichopikiwa na 'house gal'..Leo tutaangalia namna ya kupika keki ya kawaida hasa ukiwa nyumbani.
Mahitaji:
- Unga wa ngano glasi 4
- Mayai 10
- Sukari glasi 3
- Baking powder vijiko 2 vya chai
- Unga wa mdalasini kijiko 1 cha chai
- Zabibu kavu
- Maziwa fresh 1/2 glasi na mtindi 1/2 glasi
- Cocoa au kahawa
- Vanila
- tui la nazi zito kabisa,kiasi
- Mafuta 1/4 lt
- Tray ya kuokea keki yako
- Sufuria/chombo cha kuchanganyia mchanganyiko wako
Hatua za kupika:
- Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 sentigrade (365F)
- Paka mafuta kiasi kwenye kikaangio/tray yako kisha kiweke pembeni
- Pasua mayai yako kisha yaweke tkt 'brenda',weka sukari yako kisha washa mashine yako ili vichanganyike kwa pamoja hadi viwe laini kabisa.
- Weka unga wako ktk sefuria ,weka baking powder,zabibu,mdalasini,cocoa au unga wa kahawa,tui la nazi,maziwa fresh,mtindi,mafuta,vanilla,vichanganye alafu mwisho mimina mchanganyiko wako wa mayai na sukari kisha vichanganye vyote kwa pamoja hadi mchanganyiko wako uwe laini kabisa yaani uwe saizi ya kumiminika km uji.
- Chukua mchanganyiko wako huo alafu uumimine ktkt tray yako uliyoipakaa mafuta, ulioiandaa kwa ajili ya kuokea keki yako.
- Kisha uweke ktk oven kwa muda wa dk 40-45 kupika keki yako.
- Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita
- Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko
- Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga
- Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 - 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio
- Keki yako ipo tayari kwa kuliwa
Imeandaliwa na Dimamu catering Services
xxxxx---------xxxxx
Keki
ya Chocolate
Mapishi ya keki ya chocolate yapo mengi leo nawawekea pishi hili.
Mahitaji
- Unga wa ngao 250g
- Kokoa vijiko vya mezani(tbsp) 3
- Baking powder vijiko vya chai(tsp) 2
- Siagi 250g
- Sukari 250g
- Mayai 4
- Maziwa 10tbsp
Mungu akubariki sana.
Imeandaliwa na Dimamu catering Services
Nimependa sana recipe yako, hongera sana !
ReplyDeleteAsantee
ReplyDeleteJe unaset oven lako vp kwenye joto na moto
ReplyDeleteAsante kwa somo. Mie naomba msaada moto mzuri wa kuokea keki kwenye oven itoke laini bila kuungua niset ngap
ReplyDelete